NINI MAANA YA UONGOZI?
Uongozi ni mamlaka au karama ya kuonyesha njia kwa vitendo.
Kipimo cha uongozi ni jinsi gani kiongozi anaweza kuleta ushawishi kwa
watu na kufikia maendeleoyaliyotarajiwa. Kiongozi bora hana muda wa
kulalamika bali anatafuta ufumbuzi wa matatizo ya watu, yaani wananchi
au watu walio chini yake. Kiongozi wa kweli akiongea, watu husikiliza.
Maana ya uongozi
Uongozi ni dhana, taaluma inayompa mhusika madaraka na uwezo wa
kuwawezesha wale wanaongozwa naye kuunganisha nguvu, stadi na vipaji
vyao na kuvitumia ili kufikia malengo yao. Kuongoza ni kujua lengo la
wale wanaoongozwa na njia ya kufikia lengo lao.
Uongozi ni dhana,
taaluma anayopewa mhusika katika kuwaongoza wale waliohitaji kusimamiwa
au walioamuliwa kusimamiwa katika kufanikisha jambo fulani kwa maslahi
ya wote au ya mtu mmoja mmoja.
Aina za uongozi
i) Kuna njia
nyingi za kuainisha uongozi lakini njia ya msingi ni kuangalia jinsi
kiongozi alivyoingia madarakani na utaratibu wake wa kuongoza.
ii) Katika viongozi wapo Wafalme, Marais, Mawaziri, Watemi, Machifu, Wakurugenzi n.k.
iii) Viongozi hawa wote tunaweza kuwagawa katika mafungu yafuatayo
kutokana na jinsi walivyoingia madarakani na namna wanavyoongoza kama
ifuatavyo: i. Wale wanaopata uongozi kwa kurithi. ii. Wanaopata uongozi
kwa kuchaguliwa. iii. Wanaojitwalia mamlaka ya kuongoza kwa nguvu. iv.
Wanaoteuliwa na mamlaka za juu zaidi.
iv) Kiongozi anayeingia
madarakani kwa mojawapo ya njia zilizotajwa hapa juu anaweza kutumia
mtindo wake wa uongozi. Ipo mitindo mbalimbali ya uongozi: i. Uongozi wa
kimila ii. Uongozi wa kidemokrasia. iii. Uongozi wa kiimla ni mtindo wa
kuongoza ambao kiongozi huongoza kwa amri bila kushirikisha watu
wengine katika kufanya maamuzi. Mara nyingi uongozi wa aina hii haulengi
katika kukidhi maslahi ya walio wengi, bali tu ya yule anayeongoza na
wale wanaomlinda. iv. Uongozi wa kidemokrasia ni ule wa kushirikisha
watu katika kufanya maamuzi na utekelezaji wake. Kwa kawaida viongozi wa
aina hii hulenga kukidhi mahitaji ya walengwa.
NB:Viongozi
wanaochaguliwa mara nyingi huwa wanapewa muda wa kuongoza,na wale
viongozi wa wanaojiteua hujipatia wao wenyewe muda wa kuongoza au hata
hapo watakapo amua kuachia madaraka.
Sifa za kiongozi bora
i.
Awe na ufahamu. Kiongozi ni lazima awe na ufahamu mkubwa juu ya taasisi
anayoiongoza, malengo yake, mazingira na matatizo yake.
ii. Awe
mwaminifu. Kila taasisi inalenga kufikia shabaha fulani. Ni wajibu wa
kiongozi kuwaongoza wanataasisi ili wafikie malengo yao. Kwa hiyo
kiongozi ni lazima aweze kubuni mikakati na mbinu zitakazoiwezesha
taasisi anayoongoza kufikia malengo yake.
iii. Mwenye Maadili
mema. Kiongozi ni lazima akubalike katika jamii na taasisi anayoiongoza.
Ili akubalike ana budi kuzingatia maadili ya msingi ya jamii na taasisi
yake. Kiongozi mwongo, mlevi, mvivu, asiye mwaminifu n.k. hawezi kuwa
kiongozi mzuri.
iv. Amche Mungu.
v. Mwenye kukubalika na watu anaowaongoza.
vi. Mwenye kuwaongoza watu katika misingi bora ya uongozi bila kujari jinsia,rangi,ubini wala ukabila.
No comments:
Post a Comment